Mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu Tanzania, nini kimekuwa nini?


Sasa unatimia mwaka tangu Watanzania kumiminika vituoni kuchagua viongozi wao kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, na Maoni Mbele ya Meza ya Duara inauangazia mwaka huu mmoja na kile unachomaanisha kwa mpigakura wa kawaida: Je, kura yako imekuletea kile ulichokitazamia? Je, kipi kimebadilika kuwa vipi na kipi kingepaswa kuwa vipi? Vipi kuhusu suala la Zanzibar – limekwisha au bado lingalipo? Bonyeza hapa, kuungana na wachambuzi Jabir Idrissa, Rashid Chilumba na Malisa Godlisten wakiongozwa na Mohammed Khelef kwenye Maoni Mbele ya Meza ya Duara kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle. dw

 

Fungu Mbaraka ni ya Zanzibar


Nimefarajika sana kuona kwamba Wazanzibari wengi wamepata muamko mkubwa kuhusiana na maslahi ya Zanzibar katika suala la Kisiwa cha Latham (Fungu Mbaraka). Hii ni faraja kwa vile Tanganyika wameonyesha nia ya wazi, ya dhahiri na ovu katika kukichukua kwa nguvu kisiwa hichi kutoka katika milki ya Zanzibar. latham Continue reading “Fungu Mbaraka ni ya Zanzibar”

Foro: Chaka la watoto wala makombo, vijana wajifanyao machizi


Ulikuwa ni mwanzo wa usiku wa siku ya Jumanne ya tarehe 30 Agosti 2016, majira ya saa mbili na nusu, nikiwa nimeketi katika kingo za Bustani ya Forodhani, nikiwaza hili na lile. Mbele yangu kunapita kundi kubwa la watalii wa Ulaya. Nyuma yao nikaona kuna mtoto umri wa kati ya miaka 11-13. Ghafla mtoto yule anapiga ubinja (mlunzi) kumwita mwenzake wa umri wa kati ya miaka 7-8, kisha kwa pamoja wanaanza kulifuata kundi lile la watalii huku wakiwasonga kwa maneno na ishara, kuonesha kuwa wanawaomba vyakula walivyoshika mikononi mwao watalii hao.

Muonekano wa Bustani ya Forodhani kutokea jengo la Beit el-Ajab
Muonekano wa Bustani ya Forodhani kutokea jengo la Beit el-Ajab

Continue reading “Foro: Chaka la watoto wala makombo, vijana wajifanyao machizi”

CCM Zanzibar yapigana vita vya utengano dhidi ya maridhiano


Historia ya Zanzibar itamkumbuka Amani Abeid Karume kama mmoja wa viongozi waliopigania maridhiano, umoja na demokrasia visiwani humo.

Mizinga ya Forodhani

Katika kitabu chake Conversation with Myself (Mazungumzo na Nafsi Yangu), aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Marehemu Mzee Nelson Mandela, anaandika:

“Is not our diversity which divides us, it is not our ethnicity or religion or culture that divides us- since we have achieved our freedom – there can only be one division among us: between those who cherish democracy and those who do not.” Continue reading “CCM Zanzibar yapigana vita vya utengano dhidi ya maridhiano”

Sababu tatu za CUF kupigwa vita na dola


Nimeichukuwa tena na kuisoma kwa makini zaidi taarifa ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ya tarehe 15 Septemba 2016 iliyotolewa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa habari wa Bunge hilo mjini Dodoma na ambayo ilizungumzia kadhia nzima ya mgogoro wa mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.

Maalim Seif MtendeniSehemu ya taarifa hiyo ilisomeka hivi: “Tumepata taarifa kutoka kwa vyanzo vinavyoaminika serikalini kuwa kuna njama zinazopangwa na washindani wetu wa kisiasa Chama Cha Mapinduzi (CCM), vyombo vya ulinzi na usalama na serikali ya CCM kutaka kuitumia ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kumtangaza Prof. Ibrahimu Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF. Continue reading “Sababu tatu za CUF kupigwa vita na dola”

Lipumba na la kuvunda


Hufika muda tunalazimika kukubali matokeo. Inawezekana kuikubali hali hiyo kwa shingo upande au maumivu makali yasiyomithilika. Hata hivyo, maumivu na sononeko hilo haliondowi uhalisia wa mambo. Kwamba la kuvunda halina ubani hata hikima na juhudi kubwa zikitumika.

Prof. Ibrahim Lipumba
Prof. Ibrahim Lipumba

Continue reading “Lipumba na la kuvunda”

doyo

Doyo tumekusikia, tunakuhifadhia


Kuna mambo ambayo hatupaswi kuacha yapite hivi hivi pasi kuyajadili kutokana na uzito wa kile kilichojiri au mwenye kukiwasilisha kwa hadhira aliyoikusudia. Uzito wa hili la leo upo pande zote – wa mtoaji na wa kile alichokitowa, nayo ni kauli ya Katibu Mkuu wa chama Alliance for Democratic Change, Doyo Hassan Doyo, pale alipoandika kwenye ukurasa wa Facebook kuwa “Upemba ni janga la kitaifa” na hata mwandishi wa makala hii alipomtafuta kumtaka ufafanuzi, akaongeza kuwa sio tu ni janga la kitaifa, bali “Upemba ni janga la Muungano!”

Continue reading “Doyo tumekusikia, tunakuhifadhia”