HABARI

Umma Usiposema…

Wajinga ndio waliwao Waswahili walisema… Sijui kama huo msemo Wanao…maana mimi Siku nyingi duniani nimehama Na yalioko huko sinayo Na ndipo wafanyao Wanapovinjari na jeuri Wengineo wanatizama Wanyonge na wamekosa ari Kwa vitendo na zao Endelea

HABARI

Maisha, zama na zamu

Nilizaliwa mnyonge Nikakulia unyonge Lakini Nilipambana niishi Niishi waishivyo watu Watu waitwao watu Nami nikajikuta Katika mpambano huo Naingia ulingoni Nikarusha makonde Nami harushiwa pia Kwamba ndivyo maisha yalivyo Maisha zama na zamu