HABARI

‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’, kitabu kipya kuzinduliwa rasmi

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI 12 Disemba, 2009 ‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’, kitabu kipya kuzinduliwa rasmi Wapendwa Wanahabari, Ufunuo mpya juu ya uhalisia wa Mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar mwaka 1964 sasa umo kwenye maandishi. Matukio na uchambuzi wa matukio hayo, ambayo yamekuja kuubadilisha kabisa mstatili wa mambo katika dola ya Zanzibar na majirani zake unawekwa wazi… Continue reading ‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’, kitabu kipya kuzinduliwa rasmi

HABARI

Hakuna Muungano imara bila Zanzibar iliyoungana – Maalim Seif

Na Salma Said, Zanzibar SIRI zaidi za mkutano wa rais wa Zanzibar, Amani Abeid Amani Karume, na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, zinazidi kuwekwa bayana baada ya Maalim Seif kusema lengo kubwa la faragha yao ilikuwa ni kuunganisha nguvu katika kutetea mambo yanayoihusu Zanzibar kwenye Muungano. Seif alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza… Continue reading Hakuna Muungano imara bila Zanzibar iliyoungana – Maalim Seif

HABARI

Tumedhamiria kwa dhati kuijenga Z’bar mpya – Karume

Na Salma Said, Zanzibar RAIS Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume amesema yeye na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad wamesafisha nyoyo na kusameheana kwa dhati kama maadili yao yanavyowaelekeza. Akihutubia katika hafla ya baraza la Eid El-Hajj lilifanyika katika ukumbi wa Jumba la Wananchi… Continue reading Tumedhamiria kwa dhati kuijenga Z’bar mpya – Karume

KALAMU YA GHASSANI

Tatizo si Upemba, ni uelewa

Hii ni makala niliyoiandika wiki iliyopita kujibu makala ya mwandishi Abdul-Ghaffar Idrissa katika gazeti la Nipe Habari la tarehe 20 Novemba 2009 kwa jina la "Je, tatizo ni huu Upemba wetu?" Itakuwa kosa la kimantiki ikiwa makala ya Abdul-Ghaffar Idrissa ‘Je, tatizo ni huu ‘Upemba’ wetu?’ iliyochapishwa na gazeti hili wiki iliyopita, haikuchangiwa. Na, kwa… Continue reading Tatizo si Upemba, ni uelewa