No Picture
HABARI

Nacha

Nayacha macho ya wachwa, pale zama yachunzapo Nayacha kucha na kuchwa, yachecheapo nilipo Nayo yakijua yachwa, ndo uchunzi uzidipo Nacha sitachapo kucha, yachwayo nami nayacha Hamad Hamad 26 Mei 2011 Copenhagen Kutoka Kurasa Mpya

No Picture
HABARI

Nazingwa

Nazingwa ni ndugu zangu, wasonijua nilipo Waumia kwa uchungu, kila wanikumbukapo Waniombea kwa Mungu, mafanikio na pepo Numonumo ndilo langu, tenda, tarudia kuko.

No Picture
HABARI

Hunifai

Wanitaka niwe wako, ati wa ubani Niwe wako mali yako, niwewo mwandani Siliwezi penzi lako, sebu abadani Bora kaa peke yako, uwe mbali nami