Kwaheri “Baba Lao’, Allah akuridhie!

Marehemu Maulid Hamad Maulid 'Baba Lao', katika uhai wake

Leo mwandishi wa habari wa siku nyingi visiwani Zanzibar, Maulid Hamad Maulid, amezikwa kwao Bumbwini, Unguja. Maulid alifariki dunia hapo jana, baada ya kuugua kifua kikuu kwa siku kadhaa. Katika mengi ninayoweza kumkumbuka Maulid ni namna tulivyokuwa tukisalimiana kwa jina la Baba Lao, ambalo kwa hakika lilikuwa ni jina lake yeye la utani. Kila mara tulipokutana, kama sijamuona angeliniita Baba Lao nami ningelimuita hivyo hivyo, halafu tukapeana mikono na kutaniana. Alikuwa mkubwa wangu kwa umri, lakini hakuna siku aliyonifanya nijihisi hivyo mbele yake. Mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa miezi miwili iliyopita, Marikiti Kuu Darajani, nilipokuwa nyumbani kwa likizo. Allah akughufirie madhambi yako, aufanye mwema ujira wako na akuweke kwenye kundi la waja wake wema, Baba Lao! Amin!

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.