News Ticker

Tukitengana na Zanzibar tutashambuliwa’

Mbunge wa Jimbo la  Maswa Mashariki, Sylvester Mhoja Kasulumbayi

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Mhoja Kasulumbayi

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Mhoja Kasulumbayi (62), akitoa maoni yake juu ya uundwaji wa katiba mpya katika mkutano uliofanyika kwenye kata ya Ipililo iliyopo wilayani Maswa.


“Tukijitenga na Zanzibar tutaisha, watakuwa wanaingia kwenye maji na kutokea bandarini hatimaye warushe mabomu,” alisema.

MKAZI wa Kata ya Nkoma, Lazaro Daudi, amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uendelee kwani ukivunjika Zanzibar itaweza kuishambulia Tanganyika.
Alisema kuwa, kuungana kwa nchi mbili hizi kunasaidia kudumisha amani na utulivu hivyo suala hilo lidumishwe.
“Tukijitenga na Zanzibar tutaisha, watakuwa wanaingia kwenye maji na kutokea bandarini hatimaye warushwe mabomu,” alisema.

Alisema ili kuipunguzia Serikali gharama endapo rais, mbunge au diwani akifariki, mtu aliyeshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa ndani achukue nafasi yake.
Naye Kato Kiumbani (70), mkazi wa eneo hilo alitaka waruhusiwe kuachana na zao la pamba kwa kuwa Serikali hailijali
.
Wakulima wa pamba tumekuwa tukipata hasara kila mwaka, ni bora turuhusiwe kuachana na ukulima wa zao hili,”alisema Kiumbani:

“Kwa upande mwingine tangu nakua naona Serikali haitaki wafugaji, kule porini wameleta ndege wanawafukuza ng’ombe wetu wanavunjika miguu na wanakuwa wanazaa bila mpangilio, hili suala liangaliwe.”

Alisema pia kuwa, madaktari wasiruhusiwe kumiliki maduka ya dawa kwani wanatumia nafasi hiyo kuiba dawa za hospitali za umma.

“Unaenda hospitalini unaambiwa dawa hakuna halafu daktari anakuelekeza duka la kwenda kununua dawa, hii siyo sawa haya maduka yatakuwa ni yao na wanapeleka huko dawa za hospitali zetu,” alisema.

Kwa upande wake Masanja Kurwa, alitaka Katiba ijayo iwatambue wanaume waliofiwa na wake zao na kuwapa fursa ya kupata misaada mbalimbali.

“Mbona wanawake wajane wanapewa misaada lakini wanaume wakifiwa na waume zao hawapewi msaada, wanaume tuliofiwa na wake zetu na sisi tutambuliwe,” alieleza.

MWANANCHI

About Zanzibar Daima (1509 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment on Tukitengana na Zanzibar tutashambuliwa’

  1. Ndugu Lazaro,Wazanzibari ni watu waliojijengea ustaarabu wa kuishi kindugu,hii ni moja ya matunda ya kuwa na dini moja,lugha moja,itikadi na imani moja.Utumiaji nguvu kwa kujipatia maslahi ni jambo geni kwa Wazanzibari,kwa hiyo kusema wazanzibari watawahujumu kwa mabomu ni upuuzi wa mwisho.Muungano wa nchi mbili huru huja kwa ridhaa za wananchi na sio kwa mabavu.Tafuteni njia zenye maslahi kwa nchi zote mbili ili kudumisha huo muungano na sio vitisho.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s