Ofisi ya Mufti yazuia mihadhara ya upotoshaji kwa waislamu

Taarifa ya ofisi ya Mufti Zanzibar imemtaka Bibi Salama Issa Kagire mwenyeji wa Tanzania Bara ambae huja Zanzibar akidai kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kusitisha mara moja mihadharayake ya upotoshaji Waislam hapa nchini.
Taarifa hiyo iliyotolewa na kusainiwa na Kaimu Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Suleima Omar Jongo imesemakuwa Bibi Salama amekuwa akija Zanzibar mara kwa mara akiendesha mihadhara mbalimbali huku akijiita yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu jambo ambalo mafundisho ya Uislamu yanapingana nalo,
Ofisi ya Mufti ilimwita Bibi Kagire huko ofisi ya Mufti tarehe pili mwezi huu mbele ya Mufti na Sheikh Saleh Omar Kabi pamoja na jopo la maulamaa wa Zanzibar ambapo bila ya kisisi alithibitisha kauli yake hiyo ya kuudhalilisha Uislam bila ya hoja ya msingi.
Awali katika kipindi cha nyuma aliwahi kufika ofisini hapo kuomba kibali cha kufanya mihadhara ya kawaida kwa Waislamu na kuruhusiwa na hatimae waislamu kulalamikia kauli zake kuelekea kumkufuru Mwenyezi Mungu.
Alipoulizwa kuhusu hoja zake amesema kuwa antumia Qur-ani hii iliyopo na kukiri kukosewa kwa baadhi ya aya zilizomo ndani ya Qur-ni.
Kufuatia kadhia hiyo ofisi ya Mufti Zanzibar imemtaka bibi huyo kutubia na kuacha mara moja kauli zake hizo za kikafiri na endapo hatotubia  uislamu utakuja unamsuta kwa aya ya 40 ya SURATUL-AHZAAB inayoelezea kutokuja mtume mwengine ulimwenguni baada yaa Mtume Muhammad (SAW).
Pia atakosa haki zote za kisheria juu ya Uislam na kuingia msikitini na sehemu za Ibada kwake ni kharam na wafuasi wake wametakiwa kutengana fikra hizo kwani umfuata mtu huyu ni ukafiri.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotokewa na mmoja wa wafuasi wa Bibi Kagire Nd, Ahmed Suleiman Khamis mkaazi wa Darajabovu amekiri kuwepo wafuasi wa Bibi huyo anaejiita Mtume na kwa Zanzibar wapo wafuasi wapatao mia mbili.
About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

4 Comments

  1. huyo ni mgonjwa wa akili msaidieni azuiwe hospitali na aonane NA MADAKTARI WENYE ELIMU YA JUU KUHUSU UGONJWA WA AKILI HATOPONA LAKINI AKIWEKWA HOSPITALI KWA MIEZI MIWILI ATAPATA NAFUU NA AENDELEE KUTUMIA DAWA NA HAIFAI KUMCHUKULIA HASIRA HUO NI UGONJWA WA AKILI.

1 Trackback / Pingback

  1. Ofisi ya Mufti yazuia mihadhara ya upotoshaji kwa waislamu | Zanzibar Daima

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.