
Rais Mstaafu wa Zanzibar ambae pia ni Baba wa Maridhiano ya wazanzibari katika kulete Serikali ya Umoja wa Kitaifa Mh:Amani Abeid Karume jana amepata nafasi ya kutoa maoni yake ya uundwaji wa katiba mpya ya Jamuuri ya Muungano wa Tanzania kwa tume ya ukushanyaji wa maoni juu ya uundaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Mh;Karume wakati akitoa maoni yake hayo amesema kuwa hapo mwanzoni mwa Muungano huu uliopo sasa ulikuwa na heshima na kuweza kutoa usawa kwa Nchi zote mbili yaani Zanzibar na Tanganyika lakini kwa sasa kadri siku zinavokuwa zikiendelea Muungano huo umekuwa ukibadilika hatuwa hadi hatuwa na kuchukua sura mpya kwa upande mmoja wa muungano nao ni Tanganyika.
Aidha amesema kuwa wakati akiwa kama Raisi wa Zanzibar kwa kipindi cha miaka kumi iliopita ameweza kushuhudia mambo mengi sana zidi ya maslahi ya Zanzibar,aliendelea kwa kusema kuwa hivi sasa ni zama za ukweli na uwazi kutookana na hali ya Muungano iliofikisha Zanzibar hivi sasa na ili kusuluhisha hili ni kuwa na Zanzibar yenye mamlaka kamili na badae kufuatiwa na Muungano wa mkataba na yake na Tanganyika.
Heko baba wa maridhiano na dokta mwenye kukubalika ktk siasa za maelewano.
Hivyo ndovyo kiongozi anatakiwa afanye ili kuleta imani kwa wananchi, na huo ndio uongozi wenye kujali matakwa ya wananchi.
heko dk karume tupo pamoja kwa hili