Kwa Nini Wenenda Uchi?

Neuza nafsi yangu, n’kwani wawe ja hivyo
Dadie wako ne wangu, n’kwani wavaa ovyo
Utupu kwa walimwengu, wajendea vivyo sivyo
Kilowasibu nnkipi hata wemekua wehu!?

Zama zino zilopita, wekuwa watu shuwari
Wevaa hata bukuta, kujisitiri vizuri
Ila zama zilofata, wavyo dhahiri shahiri
Walisibiwa ni nini, watu hawa neuzeni!?

Wazungu walivyokuwa, myaka mia moja nyuma
Wevaa kama watawa, mavazi yao heshima
Ila leo tawajuwa, utupu hama wanyama
Ndivyo nikajiuliza, walisibiwa ni nini!?

Kishangazacho ni kino, sisi tusokuwa wao
Tu uchi hata kiuno, kitupu twezidi vyao
Majumbani ndio muno, ofisini wajazao
Kilichowasibu kipi, wakageuka wanyama!?

Othman Ali Haji
Dodoma
11 Septemba 2014

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.