LUGHA

Pumzi ‘Sinidanganye

Sinidanganye pumzi, ghururi ikanishika
Hatenda ya kipuuzi, na machafu hatamka
Nawe punde kanihizi, ubao nikafunikwa
Niwe mwenye kuonyeka, mauti yenenda nami

Sinipumbaze pumzi, hudumu wewe hakika
Nijifanyapo jambazi, chinjachinja linobaka
Punde waja usingizi, na macho yakafumbika
Na wala sitaamka, ila kwa mwanawandani

Sinighilibu pumzi, nikashindwa kukumbuka
Kumkumbuka Mwenyezi, na dhamana niloshika
Hajifanya muamuzi, wa kuusha na kuweka
Hali sina pa kushika, amali zangu madeni

Pumzi hizi pumzi, alonipa ‘tanipoka
Hata kama sikuridhi, siku yangu itafika
‘Taanguka kwenye ngazi, kisha ‘tashindwa inuka
Mola wangu akitaka, hata salamu hatumi

Mohammed K Ghassani
19 Februari 2014
Bonn

Categories: LUGHA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s