Othman Masoud atabakia daima kwenye rikodi

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Dk. Ali Mohammed Shein atakumbukwa daima ndani na nje ya Zanzibar kwa mchango wake kwa ajenda ya Zanzibar ndani ya Muungano. Aliitendea vyema nafasi yake na aliitumikia Zanzibar kwenye kiwango cha juu kabisa cha utumishi wa umma uliotukuka.

Kizuri na cha kishujaa kuliko yote ni kuwa Mwanasheria Othman hakuwa Mzanzibari aliyeufyata. Hakuwa yule ambaye akiwa Zanzibar anasema vyengine na akiwa Dodoma anayameza maneno yake akatapika yaliyo tafauti. Msimamo wake ulibakia ule ule – ndani na nje ya Zanzibar.

Zanzibar ina mengi ya kumshukuru Mungu kwa kuizawadia msomi na mwanasheria wa aina hii. Hakuiangusha taaluma yake. Hakuiangusha nchi yake.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.