News Ticker

Wanigeria wameamua, Wazanzibari wanafuatia

Dunia imesikia yaliyojiri Nigeria. Baada ya miaka 16 tangu uanze uchaguzi wa kidemokrasia hatimaye Wanigeria walio wengi wameamua kwamba wakati wa MABADILIKO (CHANGES) umewadia. Wamekipa fursa chama tawala mara tatu lakini hakuna cha maana kilichofanywa. Licha ya utajiri mkubwa wa mafuta walionao, Wanigeria walio wengi wanaishi katika ufakiri wakikosa huduma za msingi kabisa zikiwemo za maji na umeme. Ufisadi umekithiri serikalini na viongozi wameshindwa kurejesha amani na usalama nchini.

Jenerali Muhammad Buhari

Wimbo wa Wanigeria wakati wa kampeni za uchaguzi ulikuwa ni MABADILIKO(CHANGES). Na kwa kuwa wameamua imekuwa. Muhammadu Buhari, aligombea mara tatu huko nyuma, mara hii ikiwa ya nne bila ya kuvunjika moyo wala kukata tamaa, na licha ya nguvu za kijeshi za dola na hofu ya wizi wa kura, mizengwe na uchakachuaji ulotokea katika chaguzi zilizopita, kwa kuwa mara hii Wanigeria wameamua, na tena kwa KARATASI TU na imekuwa! 

Masaibu yaliyowapata Wanigeria hayakaribii wala hayafanani hata chembe na yale yaliyoisibu Zanzibar yetu azizi. Chama tawala Nigeria hakijafanya dhambi isiyosahemeka ya USALITI NA UHAINI dhidi ya nchi hiyo. Lakini Mwenyezi Mungu na Wazanzibari wenyewe ni mashahidi wa UHAINI uliofanywa na chama tawala Zanzibar wa kuiuza RASMI nchi kupitia uhalali wa kisheria wa katiba ya CCM iliyopewa jina la Katiba Inayopendekezwa.

Wazanzibari tumeshajifunza kwa Wanigeria kuwa tukiamua kwa WINGI WETU tulitakalo litakuwa, inshaa Allah. Kwa hivyo tuazimie kwa dhati kuwa tarehe 25 Oktoba 2015 tutaamua kama walivyoamua Wanigeria.

Mahaini na Wasaliti wa Zanzibar wanaeleza kwa maneno na vitendo vyao kuwa matumbo yao na chama ambacho wala si chao bali ni cha Watanganyika ni muhimu zaidi kuliko nchi yao. Sisi tuje tuwaonyeshe kivitendo tarehe 25 Oktoba kuwa ZANZIBAR KWANZA!

Mfikishie ujumbe huu kila Mzanzibari, ili yule aliyeamka aendelee kuwa macho na kwa yule aliyelala aweze kuzinduka.

Ewe Mola ipe nusra na ushindi Zanzibar dhidi ya maadui zake wa ndani na nje na uirejeshee hadhi na heshima yake pamoja na mamlaka yake kamili iliyokuwa nayo kabla ya kuanza kufisidiwa na kukoloniwa na Tanganyika, amin, amin, amin.

Waraka wa Abdulfattah Mussa 

About Zanzibar Daima (1509 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s