Linganisha mitazamo linganishi ya Kiswahili

Published on :

“Linganish! Mitazamo Linganishi Juu ya Matumizi ya Kiswahili Kiisimu, Kifasihi na Kiutamaduni” ndio maudhui kuu kwenye Kongamano la 28 la Kiswahili hapa kwenye mji wa Bayreuth, kusini mwa Ujerumani, ambalo limeanza Jumapili ya tarehe 31 Mei na litaendelea hadi Jumanne ya tarehe 2 Juni 2015 kwenye jengo la Iwalewa Haus.

Uhasidi wa wahafidhina kwa Zanzibar

Published on :

Muktadha wa makala haya ni mchakato unaoendelea wa kuipata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao sasa umebakiwa na viunzi viwili vya mwisho kukamilika – Bunge la Katiba na Kura ya Maoni. Anwani ya makala haya imekopwa kutoka jina la kitabu kiitwacho “Uhasidi wa Marekani kwa Mapinduzi ya […]

Muungano si tatizo pekee la Zanzibar

Published on :

Zanzibar ilifanya kosa kuingia kwenye mfumo huu wa muungano na jirani yake, Tanganyika. Kilichotokea Aprili 1964 ni “ajali ya kisiasa” kama zilivyo ajali nyingine zozote. Waswahili husema “ajali haina kinga”, lakini huko kutokuwa na kinga hakumaanishi kwamba ajali ni jambo zuri. Ajali zina madhara – majeraha, kuharibika mali na vyombo […]

Naam, ni Mapinduzi Daima na Zanzibar Daima

Published on :

Wazanzibari na Watanganyika wana malezi tafauti kuhusiana na sura ya Muungano. Ambapo Watanganyika wanauangalia huu kuwa ni Muungano wa Serikali Moja, Wazanzibari wanauangalia kuwa ni wa shirikisho la Serikali Tatu. Hata kama si Serikali Moja wala Tatu iliyoandikwa popote katika sheria kuu zinazoongoza sehemu hizi mbili, bado tabia, matendo na […]

Kikwete, CCM na kilevi cha Bwana Mandola

Published on :

Bwana Mandola ni mhusika kwenye filamu ya kijembe cha kisiasa iliyotolewa na Bollywood mwanzoni mwaka huu wa 2013 kwa jina la Matru Ki Bijlee Ka Mandola. Ni filamu ya vichekesho inawayozungumzia watu watatu – Harphool Singh Mandola, bintiye aitwaye Bijlee na dereva wake, Hukum Singh Matru. Bwana Mandola ana sifa, […]

Tukipima maendeleo kwa kutoendelea, hatutaendelea

Published on :

Nimerudi ziara ya wiki tatu ya nyumbani Zanzibar na nina habari njema, kwamba kote nilikopita – Pemba na Unguja – kuna dalili za kusonga mbele kama jamii, kama taifa. Kwa mfano, kisiwani Pemba nimekuta barabara inayoiunganisha miji midogo ya Mzambarauni Takao, Wingwi Mapofu, Finya na Mzambarauni kwa Kyarimu na ile […]

Donge na Pemba ni Zanzibar na zitabakia hivyo

Published on :

Wengine tutauchukulia mwezi huu wa Novemba kuwa wa aina yake visiwani Zanzibar kwa sababu ya matukio mawili, tunayoyaona ni muhimu kwa maendeleo ya kidemokrasia na kiutawala visiwani humo. Moja ni kujizoazoa kwa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) na kuja juu dhidi ya vyombo vya habari “vitakavyotumia vibaya uhuru wa habari na […]

Maalim Seif atikisa fomu urais Zanzibar

Published on :

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amechukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, huku akisema afya yake ni nzuri na yupo imara kugombea nafasi hiyo na kuongoza nchi. Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa baada ya kuchukua fomu […]