News Ticker

Mafuriko, hasara na uzembe

Kuanzia alfajiri ya jana nchi, Zanzibar, imeshuhudia mvua kubwa iliyodumu hadi mchana wake na bado inaendelea hadi hivi sasa.


Mvua hiyo imeleta madhara makubwa pamoja na kupoteza roho za watu wawili, mmoja mtoto maeneo ya nyarugusu na mwengine mtu mzima Mwanakwerekwe sokoni. Msiba mkubwa na huzuni kubwa kwa waliopoteza vipenzi vyao na kwetu sote.

Nyumba kadhaa zimejaa maji, binafsi nimeshiriki kuhamisha familia moja Migombani kwani nyumba yao maji mafutini.

Suala hili si jipya kwetu. Limekuwa likiendelea kwa miaka kadhaa. Nakumbuka miaka ya sabini mwishoni nyumba kadhaa zilikumbwa na mafuriko mitaa ya Sebleni, Nyerere na Magomeni. Nyumba hizo wenyewe walisimamiwa na serikali kuhama na kupewa viwanja maeneo mengine. Leo nyingi ya nyumba zile zimejengwa tena na kuhamiwa.

Wapi pameharibika? Usimamizi mmbovu wa serikali yetu na uelewa mdogo wa watu.

This slideshow requires JavaScript.

Wananchi wamekuwa wakionywa wasijenge mabondeni. Wakishauriwa na wanafamilia wasinunue viwanja humo lakini jambo hilo linaendelea.

Lakini pengine wananchi hawa wanafanya hivyo kutokana na ubovu wa uwajibikaji wa serikali.

Kuna maombi ya viwanja serikalini kwa maelfu. Wengi wa waombaji hawa wanapokosa hawawezi kusubiri zaidi kwani wamesubiri sana. Binafsi ombi langu la kiwanja limetimia miaka 23!

Serikali hiyo hiyo iliyowahamisha watu maeneo hatarishi inawaona wanarudi maeneo hayo pasi na kuwazuia lakini wanauwezo wa kuzuia maelfu ya watu wasihudhurie mikutano.

Serikali pia imekosa kutoa uzito katika kusimamia drainage mitaani. Misingi iliyopo haikidhi haja. Baya zaidi imejaa uchafu na takataka na kuziba. Maji hayaendi, yanatuama. Liko wapi Baraza la Mji?

Mipango miji isiyofanywa kitaalamu na majenzi yasiyokidhi haja na yasiyotathmini vipengee vya kimazingira ni tatizo la serikali, ukaguzi dhaifu. Leo Kariakoo maji tele, airport maji tele, huku na kule maji tele!

Nini kifanyike? Serikali iwajibike. Je ina nia hiyo? Sidhani.

Kama hiyo ndio hali halisi ni vema basi serikali hii iondoke madarakani. Ni wajibu wetu sote kujipanga katika kuiondosha serikali hii inayoshindwa kutekeleza wajibati zake.

Oktoba haiko mbali tuwe tayari.

Chanzo: Ukurasa wa Facebook wa Hassan Khamis, tarehe 4 Mei 2015

About Zanzibar Daima (1514 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s