News Ticker

Wageukao

Wageukao ndiyani, safari ishanogea Katikati mkondoni, chombo wakakitoboa Tuwaite jina gani, liakisi zao nia? Makuwadi? Mafatani? Katili? Maharamia?Mohammed Ghassani

Hao ni maharamia, hasidi nafsi zao
Hawajali kuumia, waumiavyo wenzao
Wajalicho kutumia, watunishe mimba zao
Hao ni maharamia
Said Shoka

Wachomoe kalafati, chombo kiende mrama
Juu sote hatupati, liliobaki kuzama
Mwenye kibega cha dhati, huyo yeye yu salama
Mohamed Ali

Mimi sitohangaika, kutafuta lao jina
Njaa yawahangaisha, la kulifanya hawana
Wenyewe wajizamisha, maji sasa watayanywa!

Mamlaka Tupumue

Hao wo wahaini, malofa maharamia
Hila zao tumaini, riziki kuparamia
Wakashindwa tuthamini, maisha kujivunia
Na wazame baharini, washindwe kuibukia
Hao ni maharamia
Abdallah Al-Alawy Baafarajiy

 

About Zanzibar Daima (1514 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s