Wageukao

Wageukao ndiyani, safari ishanogea
Katikati mkondoni, chombo wakakitoboa
Tuwaite jina gani, liakisi zao nia?
Makuwadi? Mafatani? Katili? Maharamia?
Mohammed Ghassani

Hao ni maharamia, hasidi nafsi zao
Hawajali kuumia, waumiavyo wenzao
Wajalicho kutumia, watunishe mimba zao
Hao ni maharamia
Said Shoka

Wachomoe kalafati, chombo kiende mrama
Juu sote hatupati, liliobaki kuzama
Mwenye kibega cha dhati, huyo yeye yu salama
Mohamed Ali

Mimi sitohangaika, kutafuta lao jina
Njaa yawahangaisha, la kulifanya hawana
Wenyewe wajizamisha, maji sasa watayanywa!

Mamlaka Tupumue

Hao wo wahaini, malofa maharamia
Hila zao tumaini, riziki kuparamia
Wakashindwa tuthamini, maisha kujivunia
Na wazame baharini, washindwe kuibukia
Hao ni maharamia
Abdallah Al-Alawy Baafarajiy

 

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.