DW yaanzisha ukurasa maalum wa uchaguzi wa Tanzania

Tanzania Yaamua 2015

Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle inayorusha matangazo yake kutoka mjini Bonn, Ujerumani, imeanzisha ukurasa maalum kwa ajili ya uchaguzi wa Tanzania wa mwaka huu kwenye mtandao wake.

Ukurasa huo uliopewa jina “Tanzania Yaamua 2015” unajikita kwenye kutoa habari, makala, mahojiano na matukio mbalimbali ya uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba.

Tanzania Yaamua 2015
Tanzania Yaamua 2015

Idhaa ya Kiswahili ina wawakilishi wake katika sehemu mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao wanaripoti kila mara juu ya kile kinachoendelea sasa kwenye mchakato wa uchaguzi huo ambao una ushindani mkubwa sana na ni wa kihistoria tangu taifa hilo kurejesha tena mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Kwa mengi zaidi, tembelea hapa Tanzania Yaamua 2015.

TanzaniaElectionBanner2

 

About Zanzibar Daima 1655 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply