Mwamshe Aamshikaye

Rahisi kumuamsha, aliyelala kikweli
Ila anobabaisha, kalala kumbe halali
‘Tamuamsha maisha, naye wala hakujali
Haamshwi asolala!

Asolala haamshwi, huamshwa alalaye
Mlalaji wa kughushi, yu macho kuliko weye
Ingawa hajitingishi, kulala ‘simdhaniye
Muamshe alolala!

Alolala muamshe, ikiwa yumo kwelini
Muite umtikishe, “fulani-bin-fulani”
Hata kwa maji mkoshe, ummwagie usoni
Ujuwe ataamka!

Ataamka ujuwe, na wima atasimama
Atajifuta mwenyewe, uso na wake mtima
Ila si yule ambaye, kulalakwe ni kupima
Amsha waamshikao!

Mohammed K. Ghassani
3 Disemba 2015
Dubai

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.