Ati Wewe?

Ati nani?
Nani mstahiki hishima, apawe sitara na adabu?
Wewe?
Wewe jizi, jifisadi, jihuni, wewe kyadhabu?
Hapana
Hapana wewe hufawi, hu wa nazi, hu wa tuwi, hu wa sharabu
Wewe
Wewe u jambazi, u dhalimu, wewe fasiki, wewe kisirani
Kwangu
Kwangu hupati hishima, hupati sitaha, hupati imani
‘Takwambia
‘Takwambia kila siku, kila asubuhi, kila jioni
Kwamba
Kwamba wewe u jitu duni, wewe u shetani, wewe u muhuni
Na kwalo
Na kwalo mimi nawe hatupatani, hatukubaliani, hatuendani!

Mohammed K. Ghassani
7 Disemba 2015
Nairobi

About Zanzibar Daima 1700 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply