Nakataa

Nakataa
Nakataa kukubali, kharamu kwetwa halali, hata wete walonao
Mijitutu ya bunduki
Nakataa
Nakataa sikubali, uongo kwambwa ukweli, hata wambe waambao
Mijineno malukuki
Nakataa
Nakataa kwa ukali, baya kuitwa ni zuri, lingetwa na waonao
Peke yao wana haki
Nakataa
Nakataa kullahali, haki kufanywa batili, hata kama wafanyao
Ni mijitu mifasiki
‘Mekataa
Nakataa
‘Takataa!

Mohammed K. Ghassani
09 Disemba 2015
Bonn

About Zanzibar Daima 1696 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment

Leave a Reply