Siye Tena Miye

Kama ni wewe ujaye, na mijineno ya kale, yanilevye yanivae
Kama ni wewe ambaye, mtendaji yale yale, maovu yanifanyayo nilie
Kama ni wewe uliye, ukawa nauwe vile vile, basi mimi sasa siye
Mimi siye tena yule

Yule tena mimi siye, ‘nganiona bwege duduvule, numonumo litangaye
Yule tena mimi siye, ‘nganidhani ngedere, nyama maarifa asiye
Yule tena mimi siye, na siwi tena milele, hunitendi tena weye
Naapa jina la Mungu

Naapa lake Moliwa, tukufu kubwa jinale, kiapo kino kinirejeye
Lau tena miye ‘tawa, nalivyokuwa zama zile, kukwacha unilemeye
Haviwi havitakuwa, madhali u yule yule, mimi sasa tena siye
Hunitendi tena weye!

Mohammed K. Ghassani
7 Disemba 2015

Nairobi

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.