Hakuna Kurudi Nyuma

Kwa nchi iloinuka, kisha ikaanguka, kabla ya kusimama
Kwa watu waliotoka, imara ‘kaunganika, kulinda yao hishima
Kwa chozi ‘lotiririka, hadi mwisho ‘kakauka, kuililia khatima
Kwa damu ilomwagika, mikondo ‘katiririka, ardhini ikazama
Kwa jasho ‘lilopukutika, na misuli ilochoka, kwa kazi kutwa nzima
Kwa nyuso zilokunjuka, furaha ikaripuka, kisha khofu ‘kaziandama
Kwenu nyote waadhama
Tungo hii naiandika
Nawakumbuka
Milele
Daima
Hakuna kurudi nyuma!

Mohammed K. Ghassani
10 Disemba 2015
Bonn

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.