Pigo la Mwisho

Twende na pigo la mwisho, twendeni tukaipige
Tuipige midubwasho, mchangani tuibwage
Itambuwe kuwa kesho, si yao ni ya mibwege
‘Situone legelege, hatuchi vyao vitisho

Hatuogopi vitisho, wasitutishe perege
Wangakusanya mafusho, hapa halilali zege
Tuwape pigo la mwisho, warudi wacheze nage
Kisha waje tuwaage, tuwaweke makumbusho

Mohammed K. Ghassani
12 Disemba 2015
Bonn

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.