News Ticker

Si Huru Siye na Wao

Kwa nini? Kwa nini iwe ni wao, iwe ni wao si siye Iwe watakalo liwe Lisiwe tutakalo siye Watwae lisilo lao, la kwetu walichukuwe Kisha twambwe siye nao, kweli mtu na nduguye Kwa nini?Kwa nini nguvu wapewe, nguvu hata wasonayo
Silaha wasaidiwe
Na vifaru waletewe
Kulindwa maovu yao, kusudi sisi tusiwe
Tusiwe walivyo wao, kisha bado tuambiwe –
Sote ndio hao hao
Kwa nini?

Kwa nini niulizayo, sambe sina jawabuye
Ningawa nauza leo
Yawapo kale kwa hayo
Ungajuwa hayo nawe, nayo mengi mengineyo
‘Kwa nini’ hii naiwe, kwetu na kwao zinduo
Tukikaa tutambuwe
Si huru siye na wao!

Mohammed K. Ghassani
22 Januari 2016
Bonn

About Zanzibar Daima (1509 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment on Si Huru Siye na Wao

  1. mark kandagor // January 25, 2016 at 12:44 pm // Reply

    Kazi njema kaka. Nashukuru

    Like

1 Trackback / Pingback

  1. Rais Magufuli, unaifumbia macho dhuluma na hatutakuelewa – Zanzibar Daima

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s