News Ticker

Kwa Nini?


Hivi tukueleweje?
U mjuzi wa kusema –
Au wa kweza andika?
Siasa na historia
Zetu za kwako zi jaje?
Umezificha kwa nyuma
Na kufuli ‘metundika
Wahadithia tufanyeje?
Tukupe yako heshima?
Kwa uwongo ulopika
Kwa nini?

Hivi si watuonaje?
Akili zetu ‘meduma
Au tumefadhaika?
Ufupi tuuridhia,
Huu kwetu ni upeje
Nyumbani kwetu heshima
Hiv wewe wasemaje?
Sisi ndio tulosoma
Tutakuja kuwateka
Kwa nini?

Walonga amba pwekeje
Maneno yaso maana
Hayafai kusikika
Sisi sote tunajua
Hata ikawa viweje
Simba hapigwi na kima
Atapigiwa vereje?
Simba menoye ya chuma
Si rahisi kukatika
Kwa nini??

Amour Hadji
Zanzibar
3 Februari 2016

About Zanzibar Daima (1550 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s