Mamba – II

Manju nambe, ‘siwe kama walumbao
Nigambe, nandike kwa wasomao
Niperembe, wauimbe waimbao

Huyu mamba, mjigambaji jeuri
Anatamba, adhani ana dinari
`Zondumba, zamhinika kideri

Baghairi, mi namwita mchovu
Ikidhihiri, ‘takalia kuti kavu
Msumari, utamtumbua rovu

Atatubu, atajuta kuna siku
Kulabu, zimshone zumbukuku
Uzibuzibu, umtoke ukasuku

Msimamo, shamwamba Abdilatifu
Ta’amo, afanane na nyamafu
Ungamo, atafute uongofu

  • Christopher, Budebah (Manju)
    Mwanza
    17 Feb. 2016
About Zanzibar Daima 1700 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment

Leave a Reply