News Ticker

Ya Uganda kama ya Zanzibar – Dk. Mkumbo

Yanayoendelea Uganda na sehemu zingine katika bara letu, ikiwemo Zanzibar, yatukumbushe tena kwamba Waafrika tuliupokea utamaduni wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kwa shinngo upande. Kuanzia tunavyoendesha mambo ndani ya vyama vyetu hadi katika ngazi ya taifa, ni utani unaogeuka kuwa mateso kwa wanachama na wananchi.


Bahati mbaya ni kwamba tumeiga mambo yetu karibu yote kutoka huko huko tulikoiga demokrasia, ikiwemo maana ya maendeleo!! Sasa yatupasa tutambue kwamba hayo maendeleo ya Kizungu tunayopigana kuyapata, ikiwemo dhana mpya ya uchumi wa kati, msingi wake ni demokrasia. Madamu tumeamua kuchezea demokrasia ya kimagharibi, tusahau kabisa maendeleo ya kimagharibi.

Na Kitila Mkumbo

Na Kitila Mkumbo

Hii ni kwa sababu pasipo demokrasia ya Magharibi, haiwezekani kupata maendeleo ya kimagharibi. Kama hatutaki hii demokrasia, tuachane kabisa na dhana yao ya maendeleo na tuanze kujenga dhana ya Kiafrika isiyotegemea demokrasia hii tuliyoiga kishingo upande ili tuendelee kupata misaada yao.

Lakini nawaona vijana wetu walivyojipanga kupata maendeleo ya kimagharibi na siamini kwamba inawezekana kuwashawishi waachane na hii dhana ya maendeleo. Basi nawakumbusha hawa vijana kwamba hawatafanikiwa sana kupata maendeleo ya kimagharibi kama hawatapigania demokrasia ya kweli ya kimagharibi.

Hivyo basi nawasihi vijana popote mulipo, wakati mukiendelea kupigania maendeleo ya kimagharibi, msiache kamwe kupigania demokrasia yake kwa sababu ndiyo msingi wa hayo maendeleo muyatakayo. Na tena muanze kupigania demokrasia kuanzia katika vyama vyenu.

Amini nawaambieni hatuwezi kamwe kujenga demokrasia ya kimagharibi katika nchi, bila kwanza kueneza utamaduni wa kidemokrasia ndani ya vyama vyetu. Msingi wa demokrasia katika taifa ni demokrasia katika vyama vya siasa. Wanachama wanaokumbatia vyama visivyo vya kidemokrasia, hawana uhalali wa kiroho wa kudai demokrasia katika nchi.

Huu ndio ujumbe wangu wa leo.

About Zanzibar Daima (1509 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s