News Ticker

Siku Aman Thani alipotajwa hadharani kuwa mpigania uhuru wa Z’bar

''Aman Thani ni ukurasa katika kurasa tukufu za kitabu cha Zanzibar''. - Mohammed Ghassani
Historia za Afrika zimegubikwa na historia rasmi. Historia ya uhuru wa Zanzibar haikusalimika. Historia ya Zanzibar inaanza na kumalizika kwenye mapinduzi ya mwaka 1964. Historia ya uhuru wa Zanzibar inapoelezwa na atakapotajwa Amani Abedi Karume picha itakayojengwa ni ile ya kueleza jinsi Afro-Shirazi Party ilivyokuwa ikihangaika kuwakomboa ‘’wakwezi’’ kutoka makucha ya Hizbu. Hutosikia harakati za kupigania uhuru na juhudi zilizopita za viongozi wengine kama Ali Muhsin akiongoza Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kuikomboa Zanzibar kutoka ukoloni wa Mwingereza.

AMAN THANI

By Mohamed Said

Na Mohamed Said

Nilipigiwa simu usiku muda mwingi na mtayarishaji wa  kipindi Maalum cha Mapinduzi Day akanitaka radhi na kuniomba kama nitaweza kufika Azam TV ili nishiriki katika kipindi cha kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nilikubali na hapo hapo nikaningia maktaba kuangalia nini ninaweza kusema siku ya pili katika kipindi kile. Hapo ndipo iliponijia fikra kuwa nitaongeza ufahamu wa watu wengi khasa vijana wa kizazi hiki cha sasa kama nitamueleza Aman Thani hata kwa mukhtsari kama mmoja wa wazalendo waliopigania uhuru wa Zanzibar. Nilianza kutalii nyaraka za Aman Thani na kutuma picha Azam TV ili zitayarishwe kwa kipindi tunachotarajia kukifanya siku ya pili mapema asubuhi kwenye kipindi maarufu ‘’Morning Trumpet.’’

Waliokuwa Zanzibar wanatazama Azam TV asubuhi ile waliiona picha yake kwenye televisheni kwa mara ya kwaza katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 na wakasikia historia yake.

Tafadhali hebu ingia hapa usikilize namna nilivyomleta Aman Thani katika mahojiano yangu na mtangazaji Faraja Sindegea:

Chanzo: Mtandao wa Mohamed Said, mohammedsaid.com.

 

About Zanzibar Daima (1514 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s