News Ticker

Mwanong’ona jambo gani?

Nasikia mwasemani, mungalijinong'onea  Nasikia kwa yakini, njama mnonipangia  Nasikia tambueni, kama mwataka nibwia  Mwanong'ona kitu gani, na yote nayasikia?


Mbona yaja sikioni, si kushoto la kulia 
Sauti zingawa chini, kelele zinanijia 
Mwanong’ona ndani ndani, madili kunipangia 
Mwanong’ona kitu gani, na yote nayasikia?

Naona muko shidani, mungalikinishikilia 
Mikono nitawapeni, pingu mupate nitia 
Sikio langu kichwani, hamuwezi lipatia 
Mwanong’ona kitu gani, na yote nayasikia?

Mwanong’ona ja shetani, chano anohitajia 
Mwadai mufanye nini, roho zipate tulia 
Sikizeni kwa makini, kazi bure mwajitia
Mwanong’ona kitu gani, na yote nayasikia?

Nong’ono zinong’oneni, lugha zote nazijua
Kipate kitongoeni, na Kikaye natambua
Sikio halinikhini, vizuri ladadavua
Mwanong’ona kitu gani, na yote nayasikia?

Amour Hadji
25 Februari 2016
Zanzibar

About Zanzibar Daima (1511 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s