Januari 27: Walikuwa watu, hazikuwa nambari tu

Published on :

Mwandishi nguli visiwani Zanzibar, Maalim Ally Saleh, ameandika makala makhsusi kuwakumbuka wahanga wa matukio ya Januari 26 na 27, 2001. Ni makala ambayo imeshiba taarifa za kweli na kila mwenye kuipenda na kuitakia mema Zanzibar, haachi kutiririkwa na machozi iwapo ataisoma.

Utawala unapopuuza mauaji yake ya Januari 2001 na kutuletea mazombi

Published on :

Zanzibar imejinamia. Tarehe ya leo imesadifiana na tarehe ya  miaka 16 iliyopita pale vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilipowafyatulia risasi, kuwauwa, na hata kuwatia vilema raia kadhaa visiwani Zanzibar, kufuatia maandamano ya amani yaliyogeuzwa machinjio na watawala. Kosa lao kubwa ni maandamano hayo yalifanyika katika kupinga […]

Hizi siasa si mchezo wa karata

Published on :

SAFARI moja Mei 2001, Marehemu Kanali Muammar Qadhafi, kiongozi wa Libya wa wakati huo,  alikuwa Uganda kwa ziara ya siku nne.  Alipokuwa huko alisema maneno ya kumshajiisha mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni asistaafu 2006 kama alivyotakiwa afanye kwa mujibu wa Katiba ya nchi yake ya 1995.

Tanzania: “Risasi zilinyesha kama mvua”

Published on :

Hakuna ushahidi wowote uliothibitisha kwamba waandamanaji walifanya vitendo vyovyote vya utumiaji nguvu. Hata hivyo, namna vyombo vya usalama vilivyojitayarisha kabla ya tarehe 27 Januari, inaonyesha kwamba viongozi wa ngazi za juu wa serikali na wa vyombo vya usalama walipanga na kuamrisha mashambulizi hayo mapema. Miongoni mwa wahusika walikuwa polisi, jeshi la […]

Picha kubwa ya uchaguzi wa Dimani

Published on :

Imethibiti kwamba pamoja na mikakati yote inayotumika kuhakikisha wanavunja hamasa ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), imeshindikana na bado watawala wanaendelea kuuona uthubutu ule ule wa wakaazi wa Soweto dhidi ya makaburu wa Afrika Kusini katika madai ya haki. Kila kukicha ari ya wananchi kuwaonesha wababe wachache […]

Mapinduzi yalifanyika robo siku, chinjachinja ikaendelea milele

Published on :

Ule ukarimu, ustaarabu wa Waswahili wa Pwani ulifutika kisha ukungu wa damu za wengi wasio na hatia ndio uliofunika mitaa, fukwe, viambaza na chochoro za visiwa vya Zanzibar, hasa Unguja. Siku ya tarehe 12 Januari 1964 ilikuwa ni siku ya safisha safisha ambayo haikuwahi kutokea kabla, katika historia ya Pwani ya […]