News Ticker

Juza, juvya, na julisha

Neno "juvya" si 'athari ya matamshi tu' bali ni mbadala wa "juza" na "julisha." Liko katika lahaja ya Kimvita ( na latumika mpaka hivi leo), na nafikiri  liko katika Kipemba na Kimtang'ata pia.


Kabla ya hizi harufu (herufi) za Kilatini kutumika mwishoni mwa karne ya 19 kuandikia Kiswahili, lugha hii ilikuwa ikiandikwa kwa harufu za Kiarabu, ambazo baadhi yazo Waswahili walizifanyia marakibisho (marekebisho) ili zilingane na matamshi yaliyokuwa hayakuwakilishwa na harufu za Kiarabu, kwa mfano ch, ng, ng’, p, v, na kadhalika; na pia matamshi ya kupasua yanayowakilishwa na harufu t (kama takataka), k ya kwanza kwenye neno “kuku”,  p ya kwanza kwenye neno “papa” (samaki), na kadhaliika; na pia irabu e na o.
Katika hizo harufu za Kiarabu/Kiswahili neno “jua” (kama liandikwavyo leo katika Kiswahili Sanifu), lilikuwa likiandikwa “juwa”, yaani kukitumiwa harufu ya ‘waw’, ambayo yawakilisha harufu ya ‘w’. Basi ndipo “juwa” likaweza kunyambuliwa na kuwa “juvya”; kama ambavyo twaweza kulinyambua neno “lewa” na kuwa “levya.”
Na Mwalimu Abdilatif Abdullah
About Zanzibar Daima (1514 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment on Juza, juvya, na julisha

 1. Yakubu Julius // March 8, 2017 at 12:24 pm // Reply

  Ahsante mwalimu kwa mafunzo hayo. Yanatufaa sana hakika!
  Tulikuwa na mazungumzo na Prof mmoja aitwae Assibi Amidu, ambaye anasema hivi:

  Assibi Amidu : Maelezo haya ni mazuri, ingawa, kwa maoni yangu, yamerahisishwa mno.

  Yakubu Julius: Kurahisishwa nadhani ni vyema ili tulio wanafunzi wa lugha hii tuelewe kwa wepesi, Prof Assibi Amidu

  Assibi Amidu : Taib! Lakini hatujaambiwa lolote kuhusu minyambuliko ya ‘juza’ wala ‘julisha’ wala imekwendaje hata ‘juwa’ likawa ‘juvya’. Hii ndiyo maana yangu ya awali. Pengine atayarudia maelezo haya safari nyengine. Kwa hiyo tuzidi kufuata darasa zake.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s