News Ticker

Je, wajuwa kuwa Wafaransa milioni 4 walipiga kura za maruhani?


Licha ya mgombea urais wa mrengo wa kati nchini Ufaransa, Emmanuel Macron, kujishindia asilimia 66.1 ya kura kwenye uchaguzi wa duru ya pili hapo jana, dhidi ya hasimu wake wa mrengo mkali wa kulia, Marine Le Pen, aliyepata asilimia 33.9, na ushindi huo kusifiwa kote ulimwenguni, ukweli ni kwamba kuna hatari kubwa kwenye siasa za uchaguzi nchini Ufaransa na ishara mbaya kwa Ulaya nzima.

Wapigakura 4,045,395 waliamua ama kuziharibu kura zao ama kutumbukiza karatasi tupu, yaani kupiga kura za maruhani, huku wengine 11,416,465 wakiamua kutokupiga kura kabisa. Idadi hii inatajwa kuwa haikuwa imetabiriwa na mapema na inatuma ujumbe mzito.

Ingawa kura alizopata Macron (20,257,167) ni mara mbili zaidi ya zile alizopata Le Pen (10,584,646), lakini idadi ya waliomchaguwa Le Pen anayefuata siasa kali za mrengo wa kulia ni kubwa mara mbili kuliko ile iliyomchaguwa baba yake kwenye uchaguzi wa 2002, ambaye naye alifikia duru ya pili kama bintiye. Hii inamaanisha kuwa kuna ongezeko kubwa la waungaji mkono wa siasa kali nchini Ufaransa, kama ilivyo kwenye  mataifa mengine ya Ulaya ya Magharibi.

About Zanzibar Daima (1550 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s