News Ticker

Msiimbe siasa, mtaishia pabaya – Mwakyembe

Akitilia mkazo hoja yake ya kuwa wasanii wanaoimba siasa hufikwa na matatizo, waziri huyo alimtolea mfano msanii wa Nigeria, Fella Kuti, "aliyeimba siasa na akaishia pabaya."


Waziri wa Habari wa Tanzania Bara, Dk. Harrison Mwakyembe, amewatolea wito wasanii kutokujihusisha na mambo ya siasa kwenye kazi zao, akiwaonya kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwaweka mahala pabaya.

Akijibu hoja ya Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule, ambaye pia mwanamuziki anayetambulika kwa kina la Profesa Jay, kuwa wasanii wakiimba nyimbo za siasa kuihoji serikali wamekuwa wakinyanyaswa, ila wakiimba nyimbo za kuisifia tu wanaachwa, Mwakyembe alisema kuwa wasanii hawatakiwi kuimba nyimbo za siasa na kama wanataka kuzungumzia siasa basi wagombee udiwani au ubunge.

Waziri huyo aliyewahi kuwa mwandishi wa habari na pia mwandishi wa kazi za fasihi, amewashangaza watu pale aliposema hakuna mwanamuziki yeyote duniani aliyefanikiwa kwa kuikandia serikali.

“Nimetembelea nchi kama Nigeria na wasanii waliofanikiwa kama wakina P Square, Tiwa Savage, David, ni wasanii wenye mafanikio, lakini hawajapata mafanikio hayo kwa kuitukana serikali,” amedai Waziri Mwakyembe.

“Muziki ni entartainment industry (tasnia ya burudani) na sio political indusrty (tasnia ya siasa) na hata Afrika Mashariki wasanii kama Chamilione na akina Diamond na Ali Kiba wana mafanikio lakini hawaimbi siasa,” alihoji Mwakyembe kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forum ambao umeweka vidio yake.

Akitilia mkazo hoja yake ya kuwa wasanii wanaoimba siasa hufikwa na matatizo, waziri huyo alimtolea mfano msanii wa Nigeria, Fella Kuti, “aliyeimba siasa na akaishia pabaya.”

 

About Zanzibar Daima (1509 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s