Mke atoweka baada ya kumuua mumewe kwa kisu Pemba

Atoweka na mtoto mchanga wa mkononi

Mwanamke mmoja mkaazi wa Kizimbani, Wete kisiwani Pemba, anatafutwa baada ya kutoweka na mwanawe mchanga muda mfupi baada ya kumchoma kisu na kusababisha kifo cha mumewe.

Mkasa huo ulitokea jana nyakati za Magharibi, ambapo mashahidi wanasema mwanamke huyo ambaye alikuwa mke wa marehemu kwa zaidi miaka 20 sasa, alimfuata mumewe kwenye nyumba yake nyengine, yalikotokezea malumbano na kuishia kumchoma visu miguuni mumewe.

Taarifa kutoka hospitali ya Wete alikokimbizwa majeruhi zinasema alifariki dunia majira ya saa sita na nusu usiku, kufuatia kuvuja damu kwa wingi.

 

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.