News Ticker

Haya ndiyo #MahabaMubashara: Binti Mfalme wa Japan aacha cheo aolewe


Mjukuu wa kike wa Mfalme Akihito wa Japan, Binti Mfalme Mako, amekubali kupoteza hadhi na haki zote za umalkia ili aweze kuolewa na mpenzi wake, waliyekutana tangu akiwa chuo kikuu.

Taarifa zilizotangazwa jana na kituo cha televisheni cha umma, NHK, juu ya uamuzi huo wa Binti Mfalme Mako zimeitikisa Japan nzima. Magazeti, televisheni, redio na mitandao ya kijamii imeamkia Jumatano ya leo ikiwa na habari hiyo, huku uchumba rasmi ukitazamiwa kutangazwa wiki chache kutoka sasa.

Mchumba wake, Kei Komuro, ni kijana wa miaka 25 aliyewahi kupewa jina la “Mwanamfalme wa Bahari” na mashindano ya kushajiisha utalii hivi karibuni.

Mwanamme huyo kutoka familia ya watu wa kawaida, amezungumza na waandishi wa habari muda mfupi uliopita, ambapo amekwepa kabisa kuzungumzia suala la uchumba, akisema kuwa atasema “pale tu muda utakapofika.”

Habari za uchumba huu zimezuwa mashaka makubwa sio tu juu ya nafasi ya mwanamke kwenye ukoo wa kifalme, bali pia mustakabali wa ufalme huo, ambao kwa mara ya kwanza ndani ya karne mbili zilizopita utachukuwa hatua ya kumuondoa madarakani mfalme aliye hai katika wakati ambapo warithi wa kiume ni wachache sana.

Mako, ambaye pia ana umri wa miaka 25, ni binti mkubwa wa Mwana Mfalme Akishino, ambaye ni mtoto wa pili wa kiume wa Mfalme Akihito, na kama ilivyo kwa wanafamilia wote wa kike wa ufalme huo, anapoteza hadhi na haki yake ya kifalme kwa kuolewa na mtu wa kawaida, kutokana na sheria zao.

Hata hivyo, sheria hiyo haiwahusu wanaume, ambapo Akihito na wanawe wameowa watu wa kawaida, na ambao sasa ni sehemu ya ufalme.

About Zanzibar Daima (1550 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s