Umewahi kusikia ndoa ikipandishiwa? Imetokea Zanzibar

Mwanamke mmoja visiwani Zanzibar anaripotiwa kuamuriwa na mahakama kurudi kwenye ndoa yake ya awali, baada ya kubainika kuwa ameolewa mara ya pili, akiwa bado hajaachika kwenye ndoa ya awali.

Kitendo cha mwanamke kuolewa na mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja inatambuliwa kama “kupandishia ndoa”. 

Ingawa jambo hili halikubaliki kabisa kisheria na kijamii, lakini limekuwa likitokea mara kwa mara kiasi cha sasa kuwa tishio jipya la uhai wa ndoa na familia katika jamii inayotambuliwa kuwa imelelewa kwenye misingi madhubuti ya kimaadili.
Sikiliza mkasa huu unaosimuliwa na mama mzazi wa mume ambaye mkewe ameolewa na mume mwengine akiwa bado hajaachika. 

https://m.soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/mwanamke-apandishia-ndoa-juu 

About Zanzibar Daima 1610 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.