News Ticker

Kishaanza kunuka, ACACIA yakanusha ‘kupiga’ mchanga wa madini


Moja ya kampuni zinazotajwa na ripoti ya Profesa Abdulkarim Mruma iliyowasilishwa leo kwa Rais John Magufuli, ACACIA Mining Plc, imekanusha kile kinachotajwa kuwa ni ‘wizi wa madini’ kupitia mchanga huo kwa kutokutangaza kiwango rasmi cha madini yaliyomo ndani ya mchanga huo. 


Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo katika ofisi zake za London, Uingereza, muda mfupi uliopita, inasema kuwa wakati inasubiri kuiona ripoti kamili, inajivua lawama za kutotangaza uhalisia wa kile unachokisafirisha. 

Kwa mujibu wa Profesa Mruma, kamati yake imebaini kiwango kikubwa cha dhahabu kwenye mchanga huo uitwao kitaalamu makinikia, ambapo ndani za makontena 277 yaliyozuiliwa awali bandarini na Rais Magufuli kulikuwa na tani saba za dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi trilioni 1.47.

Sio tu madini za dhahabu, bali kamati hiyo imegundua pia kuwepo kwa shaba, fedha na chuma, ambapo shaba pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi bilioni 23.3, tafauti na ripoti ya awali ya serikali iliyosema kuwa ni bilioni 13.

Kutokana na hayo, kamati hiyo imeshauri serikali isitishe mara moja usafirishaji wa mchanga nje ya nchi, sambamba na hatua nyengine kama vile kuhakikisha mitambo ya kusafishia makinikia inafungwa na kufanya kazi nchini.

Kufuatia kutolewa kwa ripoti hiyo, waziri wa madini Sospeter Muhongo tayari amepoteza kazi, sambamba na maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Madini. 

About Zanzibar Daima (1511 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s