Mchanga wa dhahabu wenda na Muhongo

Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuachia nafasi hiyo kwa hiyari yake kufuatia ripoti ya Kamati Maalum ya Kuchunguza Mchanga wa Madini kumuonesha kuwa alishindwa kusimamia ipasavyo wizara yake.

“Nimeyapokea mapendekezo yote ya kamati. Na katika hili, nimtake tu waziri asichukuwe muda mrefu aachie madaraka…”, alisema Rais Magufuli muda mchache baada ya kupokea ripoti hiyo.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Abdulkarim Mruma alisema Tanzania inapoteza kati ya Shilingi bilioni 829.4 na shilingi trilioni 1.439 kutokana na kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Profesa Mruma, kamati yake imebaini kiwango kikubwa cha dhahabu kwenye mchanga huo uitwao kitaalamu makinikia, ambapo ndani za makontena 277 yaliyozuiliwa awali bandarini na Rais Magufuli kulikuwa na tani saba za dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi trilioni 1.47.

Sio tu madini za dhahabu, bali kamati hiyo imegundua pia kuwepo kwa shaba, fedha na chuma, ambapo shaba pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi bilioni 23.3, tafauti na ripoti ya awali ya serikali iliyosema kuwa ni bilioni 13.

Kutokana na hayo, kamati hiyo imeshauri serikali isitishe mara moja usafirishaji wa mchanga nje ya nchi, sambamba na hatua nyengine kama vile kuhakikisha mitambo ya kusafishia makinikia inafungwa na kufanya kazi nchini.

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

2 Comments

  1. Contraband gold is being exported every week illegally through Zanzibar airport every week by none other than fugitive fake businessman Naushad Mohamed not less than pure raw gold 100 kilos for the last 40 years . The government of the united republic must arrest him immediately and made him not less than $ 500 million in penalties or remain in prison for the rest of his life.

  2. Dhahabu inasafirishwa kupitia uwanja wa ndege wa zainzibar na mfanyanya biashara feki Naushad Mohamed kimagendo ziadi ya kilo 100 kwa miaka arbaini sasa. Inapaswa serikali ya Muungano imshike mara mara mooja na kutaifisha mali zake zote pamoja na kutoa faini ya $ 500 millioni. mara mmoja au abakie gerezani mpaka hizo pesa zilipwe.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.