Magufuli ambwaga Mangu 

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuondosha mkuu wa jeshi la polisi, IGP Ernest Mangu, na nafasi yake kuchukuliwa na kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

Katika barua ya uteuzi wa Sirro iliyotolewa na Ikulu hivi leo, Rais Magufuli hakutowa sababu za hatua hiyo, bali amesema kuwa atampangia Magu nafasi nyengine.

IGP Mangu anaondoshwa kwenye wadhifa wakati nchi ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama, yakiwemo mauaji ya wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti, na pia sakata la mchanga wa madini unaosafirishwa nje.

Haikuwekwa wazi endapo sababu hizo ni miongoni mwa zilizomng’oa Mangu, ingawa inafahamika kuwa suala la mchanga wa madini sasa limechukuwa sura mpya, baada ya makampuni ya madini kupingana na ripoti ya Profesa Abdulkarim Mruma iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli ikionesha udanganyifu mkubwa wa makampuni hayo.

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.