Kutana na mwanamke aliyemzaa nduguye 

Mwanamke mmoja nchini Uingereza amezaa na baba yake wa kambu ili kumuwezesha mama yake mzazi kupata mtoto mwengine. 

Mama mzazi huyo, Jacky Edwards mwenye umri wa miaka 47, hakuwa tena na uwezo wa kubeba ujauzito kufuatia kuugua maradhi mabaya kwenye mimba yake ya mwisho miaka 12 iliyopita na kulazimika kufunga uzazi.

Kwa wakati huo, mama huyo wa watoto watano alifikiria kuwa asingekuwa tena na haja ya kuzaa tena. Miaka mitano baadaye, mumewe alifariki dunia, na akakutana na Paul mwenye umri wa miaka 48 mnamo mwaka 2013. 
Wapenzi hao walifunga ndoa mwaka 2014 nchini Mauritius na mwaka mmoja baadaye wakaamua kubahatisha kupata mtoto, lakini kutokana na umri wa Jacky, kliniki za kupandikiza mbegu zikakataa kuwachukuwa. 

Madaktari kwenye kliniki hizo walisema hakukuwa na fursa ya yeye kuweza tena kuzalisha mayai kwa sababu ya kukaa muda mrefu bila kupata hedhi. 

Wakati wanakaribia kuvunjika moyo, ndipo Binti wa kwanza wa Jacky aitwaye Katherine na ambaye tayari ana miaka 30 alipopendekeza kuwabebea ujauzito wao. 

“Nilifanya kwa mapenzi kwa mama yangu. Niliona namna anavyohangaika kutaka kumzalia mumewe mtoto,” anasema Katherine kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail. 

Namna hiyo ndivyo Caspian alivyokuja duniani kupitia tumbo la dada yake wa mama mmoja,  Katherine. 

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.