Barrick wamwangukia Magufuli?

Taarifa iliyosambazwa na Ikulu ya Tanzania muda mfupi uliopita inasema kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ndiyo wamiliki wakubwa wa kampuni ya Accacia, Prof. John L. Thornton, amekutana na Rais John Magufuli kwa mazungumzo ambayo yamemalizikia kwa wawili hao kukubaliana utatuzi wa mkwamo wa kiuchumi, kifedha na kisheria uliopo kati yao kwa maslahi ya pande zote mbili.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya Mazungumzo hayo Prof. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.