News Ticker

Zitto aitetea Mawio


Muda mchache baada ya serikali ya Rais John Magufuli kulifungia gazeti huru la Mawio kwa tuhuma za kuandika habari ha kuwahusisha marais wastaafu na kashfa ya mikataba ovyo ya madini, mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amekuwa wa kwanza kulitetea gazeti hilo na kuitaka serikali kulifungulia haraka. 

Akiandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto amesema uamuzi wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia. 

“Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais Magufuli mwenyewe sio Mawio. Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha”, anaandika Zitto. 

Zitto ameongeza kuwa hata kile kitendo cha Kamati ya Rais kuwatuhumu mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye mwenyewe,  Rais Magufuli, kusema “hatapona mtu” ilikuwa ni dhahiri kuwa rais huyo “anawachimba watangulizi wake.”

“Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo gazeti la Mawio lilitafsiri tu maelezo ya Rais,” anasema kiongozi huyo ambaye alinukuliwa hivi karibuni akitilia shaka uhalisia wa hatua za sasa za vita vya kiuchumi alizozitangaza Rais Magufuli. 

“Kitendo cha Rais kuonya kuwa marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘panick’ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake. Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuomba. Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.”

Serikali ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini kwetu, amemalizia Zitto kwa hashtag za #PressFreedom #UhuruWaHabari. 

About Zanzibar Daima (1550 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s