Rwanda ‘yailipa’ Sikukuu ya Eid

Katika hali isiyotarajiwa, serikali ya Rwanda imetangaza kwamba kesho Jumatatu (tarehe 26 Juni) itaendelea kuwa siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wa sekta ya umma ili kuwapa nafasi ya kuendelea kuadhimisha Sikukuu ya Eid-ul-Fitr, ambayo iliangukia katika siku ya Jumapili. 
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa leo na Waziri wa Kazi na Huduma za Umma, Bi Judith Uwizeye, inasema kuwa raia wanapewa fursa hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Rais juu ya Sikukuu za Umma. 
  

About Zanzibar Daima 1699 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.