HABARI

Rais Magufuli aifananisha Segerea na Guantanamo 

Wakati miito ikizidi kuongezeka ya kutaka serikali iwaachie viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa katika magereza ya Tanzania Bara, Rais John Magufuli amewakemea wanatoa wito huo akidai wanaonekana kuwatetea wenye tuhuma za ugaidi, huku akipiga mfano wa kushikiliwa huko na hatua ya Marekani kuwashikilia watuhumiwa kwenye gereza la Guantanamo Bay. 

Soma stori kamili kama ilivyochapishwa na gazeti la serikali la Habari Leo hapa chini:

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia waovu hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Rais amesema kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila kuyapima madhara yake.

“Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa hawa watu wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.

Msitufanye tukafika huko,” Rais John Magufuli. “Kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kuta sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule…nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani,” amesema Rais John Magufuli

“Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa waliogiza hizo uniform za jeshi,” Rais John Magufuli.

“Endeleeni kujenga heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu muda pia… mtu akifika hapa akae muda mfupi na aondoke, hata kama anasafirisha pini ifike inapokwenda na sio ipotelee njiani,”

Rais John Magufuli “Kuna vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala hawajasaini mkataba wowote.

Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyingine si watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu,” Rais John Magufuli “Sijui haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi yetu.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.