Lipumba amjibu Maalim Seif kuhusu RITA

Mwenyekiti aliyejiuzulu nafasi yake katika Chama cha Wananchi (CUF) na kisha kujirejesha katika mazingira ya kutatanisha mwaka mmoja baadaye, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema Katibu Mkuu wa hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, anapaswa kumuomba radhi kabla ya kurejea kwenye majukumu yake ofisini.

Akionekana kujibu hatua ya hivi karibuni ya CUF kufungua mashitaka dhidi ya Wakala wa Usajili wa Tanzania Bara (RITA) uliotangaza kuitambua ‘Bodi ya Wadhamini’ iliyotokana na upande wa wanachama walifukuzwa ama kusitishwa uanachama na chama hicho, Profesa Lipumba aliwaambia wafuasi wake na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu za CUF jijini Dar es Salaam kwamba wakati wa kumvumilia Maalim Seif sasa umekwisha.
Angalia video kamili hapo chini:

About Zanzibar Daima 1606 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.