HABARI

Idris Sultan aula Hollywood 

Baada ya wiki ya mchakato wa ukaguzi wa karibu, Mshindi wa Big Brother Africa-Hotshots wa 2014, Idris Sultan ataonekana katika filamu inayotarajiwa kutoka hivi karibuni ya Kimarekani ya ‘Ballin …On the Other Side of the World,’ itakayoelekezwa na Harvey White, mkurugenzi wa muziki wa Marekani na mhariri na mtengeneza filamu ambaye alifanya kazi na wasanii wenye majina makubwa baadhi yao wakiwa ni Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga na Tamia. Kama mhariri wa filamu, amehariri baadhi ya filamu kama vile ‘Think Like A Man 2,’ ‘The Wedding Ringer,’ na ‘King of the Dance Hall’ akishirikiana na Whoopi Goldberg.

 

Ikiwa imetungwa na Torino Von Jones, hadithi hiyo inamhusu kijana mdogo wa Kenya (Kunjani), ambaye wazazi wake ni waathirika wa uhalifu uliojaa vurugu. Siku moja katika maeneo ya ya shule, kijana huyo aliye na umri wa miaka kumi na tatu aligunduliwa na padri wa Kimarekani ambaye alimwona akicheza mpira wa kikapu na akaamini ana uwezo mkubwa na anaweza kushirikia ligi ya NBA. Wote wawili waliendelea na urafiki wao na padri huyo alianza kumpatia ushauri. (King) itaigizwa na  Sultan, ana haiba kubwa,lakini ni mhalifu mkubwa na hatari sana ambaye ana wazo jingine na anataka Kunjani kujiunga na kundi lake la wahalifu na atafanya kila liwezekanalo ili mpango huo ufanikiwe.
Mara ya mwisho Sultan alionekana katika filamu ya Tanzania ‘Kiumeni,’ ambayo itaoneshwa katika tamasha lijalo la wiki ya filamu la Zanzibar (ZIFF)  ambapo ‘Kiumeni’ itaoneshwa wakati wa Siku ya tamasha ya filamu za Kiswahili ya ZIFF Julai 14, na mtayarishaji na nyota wa filamu  Ernest Napoleon. Mapema mwaka huu, Napoleon aliweka historia wakati alipochaguliwa kuwa  rais wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji ya Marekani ya  D Street Media Group yenye makao yake jijini New York, pamoja na ofisi katika miji ya Berlin, Buenos Aires na Cape Town.

 

 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa D Street na mtayarishaji mtendaji Dexter Davis walimtambua Idris kutokana na kuiangalia kwa faragha filamu ya “kiumeni  huko Marekani   na alifikiria kuwa atakuwa mzuri kwa moja ya majukumu ya kuongoza. “Idris Sultan ana kile ambacho kinachohitajika ili  kuwa nyota ya kimataifa na filamu yetu ijayo ‘Ballin…On the Other Side of the World’ ameshikiri  inavyopasa kabisa. Tunatarajia Sultan kushiriki katika filamu  nyingine pia, alisema Davis. Timu yetu sasa inatazamia kupiga picha  sehemu za Marekani na Kenya na haitachelea kutafuta kipaji kikubwa  kwa waigizaji  nchini Kenya  na nchi nyingine za Afrika Mashariki  ikiwemo Tanzania pale inapolazimu.

 

 

Mazingira ya hadithi hiyo ni katika jiji la  moja ya jiji kubwa barani Afrika. Wazalishaji wanaamua nchi ya Afrika ambako uzalishaji na upigaji filamu hiyo utafanyika na wanatarajia  kufanya  upigaji picha  mwanzoani mwa mwaka mpyakuanza risasi. Dola za Marekani milioni tano zimetengwa ka ajili ya bajeti ya utengenezaji wa filamu na pia itashirikisha waigizaji wawili nyota wa Marekani ambao wataigizaji kama padri na rafiki yake mkubwa. ‘Ballin’ ni mfano mwingine wa kujitolea kwa D Street kuweka vipaji vya Kiafrika na Afrika kuoneshwa katika masoko ya soko la kimataifa. Kampuni hiyo pia ina mkono wake  katika filamu iliyojaa ‘action’ ya “Blue Mauritius,” ambayo ilipitengenezwa Cape Town na kuhusisha nyota wa filamu wa Afrika Kusini Pearl Thusi akishirikiana na  Eric Dane (Gray’s Anatomy) na John Rhys-Davies (Lord of the Rings, ) pamoja na waigizaji wengine nyota wa kimataifa kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.