News Ticker

Zaidi ya wasichana 200,000 waolewa Marekani 


Wakati mataifa tajiri ya Magharibi yakijidai kukazana kutoa mafunzo ya ustaarabu, haki za binaadamu na maadili kwa mataifa masikini duniani, ukweli ni kuwa ndani ya mataifa hayo kwenyewe kuna uvunjwaji mkubwa wa haki na maadili wanayoyapigania kwa wenzao. 

Gazeti la The Independent la Uingereza limeandika kwenye toleo lake la leo (Julai 9), kwamba zaidi ya watoto 200,000 waliolewa nchini Marekani ndani ya kipindi cha miaka 15 iliyopita, miongoni mwao wakiwemo wasichana watatu wa miaka 10 na mvulana wa miaka 11.
Ingawa umri wa chini kabisa wa kuingia kwenye ndoa katika maeneo mengi ya Marekani ni miaka 18, lakini kila jimbo lina utaratibu wake ambao hutoa mwanya kwa ndoa za utotoni kufanyika kwa sababu kadhaa, zikiwemo za ridhaa ya wazazi au ujauzito. 
Mnamo mwezi Mei, gavana wa ngazi za juu wa chama cha Republican katika jimbo la New Jersey, alikataa kusaini sheria ambayo ingelilifanya jimbo lake kuwa la kwanza kupiga marufuku moja kwa moja ndoa za utotoni kwa visingizio vyovyote. Chris Christie alidai sheria hiyo ingelikinzana na mila za kidini. 

Kwa uchache, watoto 207,468 waliingia kwenye ndoa kati ya mwaka 2000 na 2015 nchini Marekani, kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na taasisi ya Unchained At Last, ambayo inapigania upigwaji marufuku kwa ndoa za utotoni. 

Hata hivyo, idadi kamili inaweza ikawa kubwa zaidi kwani takwimu katika majimbo 10 ama hazikuwa kamili au hazikupatikana kabisa. 

About Zanzibar Daima (1514 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s