Odinga aapa kuendeleza mapambano mitaani na mahakamani

Kiongozi wa upinzani na mgombea urais kwa tiketi ya muungano wa NASA nchini Kenya, Raila Odinga, ameapa kwamba kamwe hatayatambua matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi mpinzani wake mkuu, Rais Uhuru Kenyatta ambaye, kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini humo, alipata asilimia 54 ya kura katika uchaguzi wa Agosti 8.

Akihutubia taifa kupitia mkutano wake na waandishi wa habari jijini Nairobi hivi leo, Odinga alisema yeye na viongozi wenziwe kwenye NASA hawatakubali kile alichokiita “vifaranga vya kompyuta”, akimaanisha uongozi uliopatikana kwa matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yakitolewa na IEBC kupitia mfumo wa kieltroniki na ambayo ndiyo yaliyompa Kenyatta ushindi.

Kwenye hotuba yake hiyo iliyokuwa ikingojewa kwa hamu, Odinga pia amewakosoa waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa, ambao anasema walimtolea wito wa kuyatambua matokeo ya IEBC hata kabla hayajathibitishwa.

 

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.