Balozi Seif kuzindua meli maalum ya utafutaji mafuta na gesi asilia Zanzibar

 

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kesho Oktoba 27, 2017 anatarajiwa kuzindua meli maalum kutoka nchini China ambayo itafanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia katika miamba ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi, Nishati na Mazingira Zanzibar, Ali Halil amesema meli hiyo baada ya kuzinduliwa inatarajiwa kuanza kazi rasmi katika kisiwa cha Pemba eneo la Wete na baadae kuendelea katika maeneo mengine ya Zanzibar.

Amesema meli hiyo inatarajiwa kufanya kazi hiyo kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi miwili na itatembea katika maeneo maalum kwa kuangalia miamba ambayo uchunguzi wa rasilimali hizo za mafuta na gesi utakakofanyika kwa kipindi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya habari Maelezo Zanzibar ilitolewa na Naibu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Dk Juma Mohamed Juma juu ufafanuzi juu ya zoezi hilo alisema kuwa Meli hiyo ya MV. BGP Explorer yenye urefu wa mita 64 na upana wa mita 13.8 inahusika na zoezi la Mitetemo katika bahari.

Alisema kuwa mbali ya meli hiyo pia kutakuwa na meli nyengine ambazo zitaungana nayo katika zoezi zina la utafutaji wa rasilimali ya mafuta na gesi visiwani humu.

Dk Juma alisema kuwa miongoni mwa meli hizo ni meli ya utafiti ya Fellowship yenye urefu wa mita 39.86 na upana wa mita 9.0 ambayo itakuwa na jukumu la ulinzi wakati wa zoezi la Seismic “Mitetemo” litakapofanyika.

Hiyo ni awamu ya pili ya muendelezo wa kazi ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia baadaya kukamilika zoezi la Utafutaji katika mwezi Februari, 2017 kazi hiyo ya kukagua miamba iliyoko chini ya ardhi ambapo kwa kitaalamu kazi hii inajulikana “Airborne Full Tensor Gravity Gradiometry Survey” (FTG).

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.