Wizara ya elimu Zanzibar yataja idadi ya wanafunzi waliopata mikopo ya elimu ya juu

Jumla ya Wanafunzi 1,600 wanatarajiwa kupatiwa mikopo  ya masomo kwa ngazi za shahada ya kwanza, shahada ya pili  pamoja na shahada ya tatu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Oktoba 26, 2017 huko ofini kwake Mazizini nje kidogo ya  Mjini wa Zanzibar, alisema kuwa idadi ya wanafunzi hao imepatikana kwa mujibu wa bajeti ya Serikali ya Zanizibar kwa mwaka 2017-2018.

Alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya utoaji wa mikopo hiyo   jumla ya waombaji 1,021 kati fomu za maombi 2,675 zilizotolewa katika vituo vya Unguja na Pemba, kwa ngazi mbali mbali za elimu ya juu tayari wameshateuliwa kwa ajili ya kupatiwa mikopo hiyo.

Aidha ameongeza kuwa kati ya wanafunzi hao walioteuliwa awamu ya kwanza kupatiwa mikopo hiyo wanafunzi wa Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) wapo 983, Shahada ya Uzamili (Master Degree) 34 pamoja wa Shahada ya Uzamivu (Doctor of Philosophy – PHD) wanafunzi 4 tu.

Alisema kuwa jumla ya shillingi milioni 64,000 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kulipia gharama za masomo kwa wanafunzi hao waliopata ufadhili kutoka Serikali ya Zanzibar katika masomo yao ndani ya vyuo vikuu vya Tanzania.

Amefafanua kuwa gharama hizo zinajumuisha malipo ya ada ya masomo, mitihani, posho la kujikimu, posho la vitabu, posho la mafunzo ya vitendo pamoja na mahitaji maalum ya vitivo vyao.

Waziri Pembe alisema kuwa kuwa uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa vigezo mbali mbali pamoja na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kutoka 50 hadi kufiki 88 kwa mwaka 2017.

Hata hivyo metoa wito kwa wale waombaji ambao hawakuteuliwa kwa awamu ya kwanza wawe na subira kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inaendelea na awamu nyengine za uteuzi ambapo teuzi za majina ya waombaji wa mikopo zitafanywa kwa kadiri ambavyo Kamisheni ya Vyuo Vikuu ya SMT (Tanzania Commision for Univversities – TCU) itakapotangaza majina mapya ya wanafunzi watakaopatiwa udahili katika vyuo vikuu na taasisi nyengine za elimu ya juu hapa nchini.

About Zanzibar Daima 1611 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.